HISTORIA
Upya kiroho, ni kundi ya Karismatiki katoliki lililo na makao yao Marekani. Kundi hili lilianzishwa na vijana watatu mwaka 2016, Jean Claude Kibaba, Josephine Biringanine na Asani Pierre Ekyoci. Washiriki walihanza kukutana kwa njia ya simu na kuendesha maombi ya Karismatiki Kikatoliki kwa lugha ya Kiswahili. Leo wakristu wengi Wakatoliki warungumzao Kiswahili kote ulimwenguni ( Usa, Kanada, Ulaya na Australia) wananufaika na mpango huu kwa kujiunga pamoja kupitia simu au mtandao.
HUDUMA ZETU
Tunazingatia ushirika na Mungu kwa kupitia na kueleza nguvu na karama za roho mtakatifu katika maisha yetu na ndani ya kanisa. Wakati wa mikutano ya maombi tunamsifu, kumtukuza na kumwabudu Mungu
DHAMIRA YETU
Malengo katika kanisa ni pamoja na:
kuwatia moyo Wakristo, kuishi maisha ya maombi, mafungo na kitume.
Kukuza wongofu wa kibinafsi kwa Yesu Kristo, na ubatizo wa Roho Mtakatifu
Kufundisha na Kudumisha imani na tamaduni za kanisa